Concluded cases

TAARIFA YA MALALAMIKO  YALIYOWASILISHWA NA SEKRETARIETI YA MAADILI  YA VIONGOZI WA UMMA  MBELE YA  BARAZA LA MAADILI MWEZI  APRIL NA JUNI, 2011

1.0 Utangulizi:

Awamu ya kwanza ya  vikao vya Baraza la Maadili  kusikiliza malalamiko dhidi ya viongozi wa umma  ilianza rasmi   tarehe 11-18 April, 2011. Jumla ya malalamiko 21 yaliwasilishwa na Sekretarieti ya Maadili mbele ya Baraza.  Aidha, Baraza lilitoa maoni na mapendekezo yake kwa mujibu wa matakwa ya fungu la 22(6)  likisomwa pamoja na fungu la (8) la  Sheria ya Maadili Na. 13 ya mwaka 1995 (Sura 398). Matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Baraza yanaainishwa katika Jedwali A hapo chini:-

Jedwali A: Matokeo ya malalamiko yaliyofikishwa mbele ya Baraza la Maadili  kwa awamu ya kwanza, mwezi April, 2011.  

Idadi viongozi waliofikishwa mbele ya Baraza

Aina ya malalamiko

Maoni na mapendekezo ya Baraza

21

Kutowasilisha Matamko ya Rasilimali na Madeni.

Onyo

Onyo kali

Hana hatia

10

3

8

 

1.1  Idadi ya malalamiko yaliyowasilishwa mbele ya Baraza la Maadili  kwa awamu ya Pili.

 Katika awamu ya pili  Baraza  lilitarajia kusikiliza jumla ya malalamiko 30. Kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo,  ni malalamiko 22   yaliyofikishwa mbele ya Baraza. Aidha, Baraza lilisikiliza malalamiko 20 na malalamiko 2 yaliahirishwa.  Mchanganuo wa Idadi,  aina ya malalamiko na maoni na mapendekezo ya Baraza kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa  ni kama inavyofafanuliwa hapo katika jedwali B:

Jedwali B: Matokeo ya malalamiko yaliyofikishwa mbele ya Baraza la Maadili mwezi Juni, 2011

Idadi ya viongozi waliofikishwa mbele ya Baraza

yaliyohairishwa

Aina ya malalamiko

Maoni na Mapendekezo ya Baraza

22

2

Kutowasilisha Matamko ya Rasilimali na Madeni  na lalamiko moja lilihusu matumizi Masaya ya madaraka

Onyo

Onyo kali

Hana hatia

4

7

9