Gallery

[0 Photos]
Feb 25,2016 Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma chini ya Ufadhili wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Kimataifa la Marekani USAID liliendesha semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano. Semina hiyo ilifunguliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ilifanyika Ikulu jijini Dar es salaam

[0 Photos]
Januari 01, 2016 Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Ombeni Sefue walitia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu ya Viongozi wa Umma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. John Magufuli, Makamu wa Rais mhe. Samia S. Hassan na Waziri Mkuu mhe. Kasim Majaliwa. Ahadi ya Uadilifu ni tamko rasmi na bayana la dhamira ya kuwa na mwenendo wa kimaadili na kuunga mkono Kampeni ya Kitaifa ya Maadili na Mapambano dhidi ya Rushwa. Ni Hati ambayo inaruhusu Kampuni au Afisa wa Umma kutoa ahadi ya kuzingatia Kanuni za Maadili na Mkakati wa Mapambano dhidi ya Rushwa katika Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Tanzania. Viongozi wa Umma na Watumishi wa Umma wote wanaofanyakazi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makampuni yaliyosajiliwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatakiwa kutia saini hati hiyo ya Ahadi ya Uadilifu

[6 Photos]
Januari 05,2016 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki alifanya ziara katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Makao Makuu Dar es salaam na kupata nafasi ya kuzungumza na Menejimenti na baadhi ya watumishi wake. picha zifuatazo zinaonyesha ziara hiyo

[0 Photos]
Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma iliendesha mdahalo uliojumuisha wadau wake mbalimbali kuadhimisha Siku ya Maadili Duniani (Dec 10, 2015), mdahalo huo ulifanyika katika Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Fuatilia picha zifuatazo kuona ilivyokuwa