Events

 • Elimu kwa umma kwa njia ya Redio mkoani Tabora
  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imekuwa ikitoa elimu kuhusiana na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya 1995 ili kuweza kueleweka kwa viongozi ili kuitekeleza na kwa wananchi kwa ujumla ambao ni wasimamizi. Hivi karibuni katika kutekeleza jukumu la kutoa elimu , Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi iliendesha vipindi vya redio kupitia Redio ya Voice of Tabora Maswali hayo yamekuwa yakiulizwa na wananchi mbalimbali na sio viongozi pekee, kutokana na hali hiyo leo tunawaletea maswali na majibu hayo kama ambavyo yalivyoulizwa na wananchi mbalimbali na majibu yake kama yalivyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi - Tabora ili kuwafahamisha wananchi wengi zaidi kupitia tovuti yetu.
 • SEMINA YA MAADILI KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA
  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imekuwa ikitoa elimu kuhusiana na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya 1995 ili kuweza kueleweka kwa viongozi ili kuitekeleza na kwa wananchi kwa ujumla ambao ni wasimamizi. Hivi karibuni katika kutekeleza jukumu la kutoa elimu , Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati iliendesha mafunzo kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo maswali mbalimbali yameulizwa na waheshimiwa Madiwani. Maswali hayo yamekuwa yakiulizwa na wananchi mbalimbali na sio viongozi pekee, kutokana na hali hiyo leo tunawaletea maswali na majibu hayo kama ambavyo yalivyoulizwa na madiwani hao na majibu yake kama yalivyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati- Dodoma ili kuwafahamisha wananchi wengi zaidi kupitia tovuti yetu.
 • Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala yatembelea Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala wametembelea Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Makao Makuu jijini Dar es salaam na kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.
 • AZAKI ZAPEWA RUZUKU KUKUZA MAADILI NCHINI
  Asasi za kiraia tatu zimepewa ruzuku ya sh milioni 30 kila moja na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma nchini kupitia mradi wa ufadhili wa USAID kwa lengo la kuimarisha kazi ya kusimamia na kukuza maadili nchini. Azaki hizo ni TACOSODE, BAKWATA KISARAWE na Chama cha Wastaafu wa Kisarawe.
 • Vipindi vya Elimu kwa Umma kupitia TBC Taifa Redio
  Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma inarusha vipindi vya redio tbc taifa kila siku ya Jumanne kuanzia saa 9.15 hadi 9.45