Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili Kanda ya Kati –Dodoma Bibi. Jasmin Awadh akitoa mada kuhusu maadili kwa watumishi wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za EWURA Jijini Dodoma tarehe 25 Julai 2022.

Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakifuatilia kwa makini mada kuhusu Maadili iliyowasilishwa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili kanda ya Kati-Dodoma Bi. Jasmin Awadh. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ofisi za EWURA Jijini Dodoma tarehe 25 Julai 2022.

Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi (hayupo pichani) akiongoza kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi mbalimbali walioteuliwa hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Simon Sirro pamoja na Inspekta Jenerali wa polisi ( IGP) Camillius Wambura. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai 2022.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mkwakwani Jijini Tanga ambao ni wanachama wa klabu ya Maadili wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokua zikitolewa na Maafisa kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (hawapo pichani). Mafunzo hayo yalifanyika shuleni hapo hivi karibuni.

Katibu idara ya usimamizi wa maadili Bwana John Kaole akifafanua lengo la watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutembelea kituo cha watoto yatima cha kijiji cha Matumaini kilichopo Jijini Dodoma tarehe 23 juni 2022.

Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi akitoa maelezo kuhusu Majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa baadhi ya watumishi wa mahakama Kuu Jijini Mwanza alipokua kwenye ziara ya kikazi mkoani humo tarehe 17 June 2022. Kushoto kwa Kamishna ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Mkoani Mwanza Mhe. Wilfred Peter Dyasobera na kulia kwake ni Mhe. Jaji Kasim Robert.

Baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu mkoani Mwanza wakimsikiliza Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi (hayupo pichani) akijibu maswali mbali mbali yaliyohusu Tamko la Mali na Madeni kwa Viongozi wa Umma alipotembelea Mahakama hiyo Juni 16,2022

Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi ( katikati kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza mara baada ya kikao chake na Viongozi wa Umma wa Mkoa huo katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma . Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo tarehe 16 Mei 2022.

Karibu


Sekretarieti ya Maadili ni Idara ya huru ya Serikali chini ya Ofisi ya Rais iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 132 ya Katiba ya 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi yake kuu ni kutekeleza Sheria ya Maadili ya Uongozi wa Umma, Na. 13 ya 1995 (Sura ya 398), hasa kufuatilia tabia na maadili ya Viongozi wa Umma. Tovuti hii ni njia ya habari muhimu juu ya kukuza na kutekeleza kanuni na maadili ya kimaadili ambayo ni lazima ya kuzingatiwa na Viongozi wote wa Umm... Soma zaidi

 • news title here
  26
  Jul
  2022

  Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji ( EWURA) watakiwa kuzingatia misingi...

  Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji ( EWURA) watakiwa kuzingatia misingi ya maadili... Soma zaidi

 • news title here
  23
  Jun
  2022

  Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili wahitimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutembelea...

  Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili wahitimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutembelea kituo cha watoto yatima... Soma zaidi

 • news title here
  22
  Jun
  2022

  Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili waadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma Kitaifa kwa kup...

  Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili waadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma Kitaifa kwa kupanda miti... Soma zaidi

Habari Zaidi
  • 27
   Jul
   2017

   Sekretarieti ya Maadili yaadhimisha Siku ya Maadili.

   Mahali: At Mnazi Mmoja Stadium

   Soma zaidi
  • 29
   Jul
   2017

   maadili siku ya michezo

   Mahali: Gymkhana Ground

   Soma zaidi
  • 25
   Jul
   2017

   Warsha ya Wahariri wa Vyombo vya Habari

   Mahali: Serena Hotel

   Soma zaidi
  • 25
   Jul
   2017

   Baraza la Maadili

   Mahali: Karimjee Hall

   Soma zaidi
  Matukio Zaidi