Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakiimba wimbo maalumu wa wafanyakazi (solidarity) wakati wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha, tarehe 20 Machi 2024.
Kamishna wa Maadili na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha, tarehe 20 machi 2024.
Kamishna wa Maadili na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi akifurahia jambo na Katibu wa Baraza la wafanyakazi, Bi. Subira Kaporo (wa kulia) pamoja na mjumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi, Dr. Leonia Msafiri kabla ya kuanza kwa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha, tarehe 20 Machi 2024.
Baadhi ya maafisa uchunguzi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakifuatilia mada mbalimbali zinatolewa wakati wa kikao kazi cha uchunguzi kilichofanyika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha, tarehe 18 Machi 2024.
Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi akiongea na maafisa uchunguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kikao kazi cha wachunguzi Kilichofanyika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha tarehe 18 Machi 2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiongea na maafisa uchunguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kikao kazi cha wachunguzi Kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha tarehe 18 Machi 2024.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara SACP. George Katabazi akishuhudia kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi mbalimbali wa Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara Kiapo hicho kiliongozwa na Bw. Gerald Mwaitebele Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Kaskazini. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 14,03,2024 Katika Ukumbi wa wa Polisi Mess Manyara.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst) Sivangilwa Mwangesi (hayupo pichani ) akiongoza kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi mbalimbali walioteuliwa hivi karibuni. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2024.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakifuatilia taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo hilo iliyofanyika tarehe 13 marchi 2024, jijini Dodoma
Katibu Idara ya Usimamizi Maadili, kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Bw. John Kaole akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili kwa waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali wakati wa ziara ya ukaguzi wa jengo hilo. Ziara hiyo iliyofanyika tarehe 13 machi 2024 jijini Dodoma.