Daftari la Vihatarishi la Sekretarieti ya Maadili kuhuishwa.


Daftari la Vihatarishi la Sekretarieti ya Maadili  kuhuishwa.
12
Oct
2021

Daftari la Vihatarishi la Sekretarieti ya Maadili kuhuishwa.

Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ambao ni Vinara wa Vihatarisi “Risk Champions” kutokamakao Makuu na Kanda kuhuisha daftari la vihatarishi la Taasisi la mwaka 2021/2022. Zoezi hilo limefanyika katika kikao kazi cha watumishi hao kilichofanyika Mjini Morogoro mapema wiki hii.

Akifungua kikao kazi kazi hicho Kamishna wa MaadiliMhe. JajiSivangilwa Mwangesi alisema kuwa kikao kazi hicho kina lengo la kuhuishadaftari hilo ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mwongozo kutoka Wizara ya Fedha na mipango chini ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, ambapo inatakiwa kila Taasisi za Umma kuhuisha madaftari ya vihatarishi.

Mhe. Mwangesi alisema kuwa Ili kuhakikisha Sekretarieti ya Maadili inafanya kazi zake ipasavyo kwa ufanisi lazima Taasisi ifuate Sheria,Taratibu na miongozo inayotolewa katika kutekeleza majukumu yake.”hatuna budi kufanya kazi hii ya kuhuisha daftari la vihatarishi kwani ni agizo kutoka juu nasi tupo kwa ajili ya utekelezaji”

Aidha Mhe. Mwangesi aliwaasa watumishikufanya kazi kwa kujituma, kufuata sheria, Kanuni na taratibu ili kuifanya Sekretarieti ya Maadili iweze kusaidia Serikali katika kutimiza malengo yake.”Nasisitiza kuhakiksha mnaelewa na kuvifanyia kazi vipengele vinavyohusiana na masuala ya vihatarishi kwa ujumla wake ili muweze kutekeleza kwa ufanisi kazi hii”alisisitiza Mhe. Mwangesi.

Mhe. Mwangesi aliongeza kuwa ni jukumu la kila mmojakatika kazi hii kushiriki ipasavyo na kuzingatia yale yote yatakayowasilishwa na mwezeshaji ili sote tuwe na uelewa wa vihatarishi vya Taasisi.

Aidha kikao kazi hicho mbali na kuhuisha daftari la Taasisi lamwaka2021/22 wajumbe walipata wasaa wa kupitia na kuchambua namna nzuri na bora ya uandaaji wa Uchambuzi wa vihatarishi, mpango wa kudhibiti vihatarishi namwongozo wa kudhibiti vihatarishi katika Taasisi.