Mkuchika awapongeza Watumishi wa Umma.


Mkuchika  awapongeza  Watumishi wa Umma.
12
Dec
2019

Mkuchika awapongezaWatumishi wa Umma.

Waziri wa NchiOfisiyaRais, Menejimentiya Utumishi wa Ummana Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (Mb) alisema kuwa kiwango cha utendaji kazi katika Utumishi wa Ummakimeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na kipindi cha hapo nyumakuwapongeza watumishi wote wa Umma kwa kufikia hatua hiyo.

Mh Mkuchika aliyasema hayo katika kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu lililofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika aliwataka Watumishi wote wa Umma Kufanya kazi kwa Uadilifu, Uwazi na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumisi wa Umma wakati wa kutekeleza majukumu yao.Aidha,kupitia kongamano hilo, Mhe. Mkuchika alisema kuwa Maadhimisho ya siku ya Maadili yatawasaidia watumishi wa Umma kuboresha mienendo yao katika utekelezaji wa Majukumu yao ya kila siku. Na pia itasaidia kuleta mabadiliko chanya kwa watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za BinadamuKamishna wa Maadili Mh Harold Nsekela alifafanua kuwa, suala la Maadili ni suala la Kikatiba na Kisheria na kwamba viongozi pamoja na watumishi wa umma hawana budi kulitekeleza kwa umakini na kwa uadilifu mkubwa.

“KwaViongozi na watumishi wa umma tunatakiwa kuwa mfano wakuigwa katika kukemea vitendo vya utovu wa Maadili ikiwemo rushwakwa wale tunaowaongoza na jamii kwa ujumla, tusingoje kunyooshewa vidole.” Alifafanua Mhe. Nsekela

Mhe. Nsekela alifafanua kuwa, kupitia Kongamano hili muhimu ni wakati mzuri kwa watumishi wa Umma na Viongozi kwa ujumla kujipima utendaji wao wa kazi na pia kujirekebisha pale wanapokosea.

Katika hotuba yakeMhe. Nsekelaalibainisha kuwa, maadhimisho haya, huadhimishwa kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambapo alisema lengo kuu la maadhimisho hayo likiwa ni kupinga vitendo vya rushwa.

Aliongeza kuwa,Maadhimisho haya hufanyika Desemba 9 kila mwaka, lakini Tanzania ilisogeza mbele hadi Desemba 10 ili kupisha sherehe za Uhuru ambazo hufanyika Desemba 9kila mwaka.

Maadhimisho hayo yalishirikisha jumla ya Taasisi za Umma 9 ambazo ni Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais - Ikulu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka yaUdhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Sheria na Katiba na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT).