Rais John Pombe Magufuli arejesha tamko la rasilimali na madeni kwa Kamishna wa Maadili.


Rais John Pombe Magufuli arejesha tamko la rasilimali na madeni kwa Kamishna wa Maadili.
30
Dec
2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasilisha tamko linalohusu Mapato, Rasilimali na Madeni ya viongozi katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kikatiba na kisheria.

Tamko hilo limewasilishwa tarehe 29 Desemba, 2019 katika ofisi hizo kanda maalumu ya Dar es salaam na katibu wa Rais, Bwana Ngusa Samike ambaye ametumwa na Mhe Rais ambaye yuko mapumzikoni Chato, mkoani Geita na limepokelewa na Kamishna wa Maadili Jaji (Mst.) Harold Reginald Nsekela.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea tamko hilo Kamishna Nsekela amesema kitendo alichokifanya Mhe. Rais kimetekeleza takwa la kikatiba Ibara ya 132 (5) (b) linalowataka viongozi kuwasilisha taarifa za tamko la mapato, rasilimali na madeni mara kwa mara lakini pia ametekeleza sheria Na. 13 ya mwaka 1995 kingu cha 9.

Wakati huo huo, Jaji (Mst.) Nsekela alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wengine kutumia siku mbili zilizobaki kufanya hivyo kabla ya tarehe 31 Desemba katika kutekeleza takwa hilo la kikatiba na kisheria.