Viongozi waaswa kusimamia Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu.


Viongozi waaswa kusimamia Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu.
11
Dec
2020

Viongozi waaswa kusimamia Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu.

Viongozi wote wanaosimamia utoaji wa huduma katika Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wanapaswa kuwajibika na kusimamia ipasavyo utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwenye maeneo yao.

Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katikakilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Katika Hotuba yake Mhe. Pinda alisema kuwa “Natambua kuwa miongoni mwenu wapo wachache ambao wamejawa na ubinafsi na hivyo kujihusisha na vitendo vya Rushwa na hivyo kuwakosesha wananchi haki zao”.

“Natoa wito kwa viongozina wadau wengine kuhakikisha kuwa Ahadi ya Uadilifu na Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa vinazingatiwa ipasavyo katika Taasisi zenu zote” alisisitiza Mhe. Pinda.

Mhe .Pinda aliongeza kuwaAhadi ya Uadilifu kwa Sekta Binafsi inawataka watumishi wa sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika kuchangia ukuaji wa Uchumi wa Taifa kwa njia ya kulipa kodi kutokana na shughuli zote za kibiashara kwa njia ya uwazi na uadilifu, kutoshawishi, kuomba au kutoa rushwa au hongo au aina yoyote ile ya rushwa. Pia, kuhakikisha kuwa mfumo wa kutoa taarifa za mapato ni wa uwazi na hauruhusu kamwe vitendovya rushwa na utovu wa maadili katika manunuzi ya umma.

Aidha, Mhe. Pinda aliwakumbusha watumishi wa umma msimamo wa Rais wetu wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu watumishi wa umma walio wazembe na wasio waadilifu kuwa hawana nafasi katika serikali yake anayoiongoza jambo lililoifanya nchi yetu kusifiwa na mataifa mengine kwa hatua inazozichukua katika kuimarisha Uadilifu na Vita Dhidi ya Rushwa.

“Hakika huu ni wakati mzuri sana wa kubadilisha mitazamo ya Watanznia na kuwafanya waamini kuwa Tanzania yenye watumishi waadilifu, wapinga rushwa na wazalendo inawezekana” alisema Mhe. Pinda.

Pamoja na hayo Mhe. Pinda alisema kuwaSerikali imefanya jitihada nyingi katika kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unajengeka na kuwa wa kutegemewa na ummakwa kutungwa kwa sheria mbalimbali za usimamizi wa utendaji wa watumishi kama vile Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake; Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma; Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma;Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Miongozo mingine ya kiutumishi yoote hayo ikiwa na lengo la kuboresha Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe. Pinda alitumia fursa hiyo kuwaasa Watumishi wa Umma na Walioko katika Sekta Binafsi kwamba wananchi ndio waajiri wao hivyo kila mmoja katika nafasi yake awahudumie ipasavyo na kwa weledi wa hali ya juu.

Aidha Mhe. Pinda aliwashukuru wabia wa Maendeleo kwa mchango wao katika kufanikisha utekelezaji wa mikakati ya kitaifa hususan katika nyanja ya usimamizi wa utoaji haki na katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.

“Nimejulishwa kuwa Mradi waBuilding Sustainable Anti-Corruption Action of Tanzania(BSAAT) unaofadhiliwa na Shirikala kimataifa la maendeleo la Uingereza (Depertment for International Development_ DFID) unatekelezwa kwa ufanisi mkubwa” alisema Mhe Pinda.

Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu huandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi na Taasisi zenye dhamana ya masuala ya Utawala Bora, Maadili, Udhibiti wa Rushwa na Usimamizi wa haki za Binadamu ambazo ni :Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Katiba na Sheria,Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa, Sekretarieti ya Maadili Viongozi wa Umma, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali, Mamlaka KudhibitiUnunuzi wa Umma, Tume ya Utumishi waUmma na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Maadhimisho hayo mwaka huu yalifanyika kwa kongamano lililohusisha taasisi zisizo za kiserikali pamoja na wabia wa maendeleo na kauli mbiu ilkua “ Uzingatiaji wa Ahadi ya Uadilifu kwaViongozi na Watumishi kwa Ustawi wa Utawala Bora na Haki za Binadamu nchini’