Viongozi wametakiwa kusimamia Sheria ya Maadili katika utekelezaji wa majukum yao.


Viongozi wametakiwa kusimamia Sheria ya Maadili katika  utekelezaji wa majukum yao.
26
Jun
2019

Viongozi wametakiwa kuzingatia Sheria ya Maadili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Viongozi wametakiwa kusimamia Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Harold Nsekela katika mkutano na Viongozi wa Umma kuhusu Maadili uliofanyika mkoani Dodoma.

Mhe. Kamishna alisema kuwa Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti mgongano wa maslahi katika maeneo yao ya kazi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge ambae ndiye aliyekua mgeni rasmi kwenye mkutano huo alisema kuwa Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa na utashi na utayari wa kufanya kazi kwa uadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Mhe. Mahenge alifafanua kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli imekua katika mstari wa mbele katika kusimamia uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika utekelzaji wa majukumu yao kwa kuweka mbele maslahi ya Umma kuliko kuweka mbele maslahi yao binafsi.

Aidha Dkt Mahenge aliongeza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi kutambua nafasi aliyo nayo kama Kiongozi katika kupiga vita suala la mgongano wa maslahi.

Pia Mhe. Mahenge alizidi kuwaasa Viongozi hao kutumia dhamana yao ya Uongozi waliyopewa kudhibiti mgongano wa maslahi katika maeneo yao ya kazi ili kuondoa vitendo vya rushwa pamoja na vitendo vingine ambavyo ni vya uvunjifu wa maadili vinavyopelekea kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

Mkutano huo wa siku moja uliandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa nia ya kuwakumbusha Viongozi wanaohusika na sheria ya Maadili kusimamia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.