Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ‘wapigwa msasa’ Ujazaji Fomu kwa njia ya Mtandao.


Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili  ‘wapigwa msasa’  Ujazaji  Fomu  kwa  njia  ya  Mtandao.
21
Jul
2020

Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili Makao Makuu na Kanda ya Kati ‘wapigwa msasa’UjazajiFomukwanjiayaMtandao.

Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili wametakiwa kuendelea kuufanyia mazoezi kwa vitendo Mfumo wa Ujazaji Fomu kwa njia ya Mtandaoili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwasaidia viongozi wa umma watakapo kuwa wakijaza matamko yao kupitia mfumo huo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Kipacha katika ufunguzi wa mafunzo mafupi kuhusu ujazaji wa matamko ya rasilimali na madeni ya viongozi kwa njia ya mtando yaliyotolewa kwa Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili, Makao Makuu na Ofisi ya Kanda ya Kati - Dodoma yaliyofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 21 katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili Makao Makuu Jijini Dodoma.

Katika hotuba yake Bw. Kipacha aliongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Matamko ya Rasilimalina Madeni ya Viongozi wa Umma yamekuwa yakijazwa na kuwasilishwa Sekretarieti ya Maadili kwa nakala ngumu ya Fomu, zoezi ambalo limekuwa na changamoto nyingi ikiwemo gharama kubwa na muda mwingi kutumika katika kutuma fomu hizo.

Aidha,Bw.Kipacha alifafanua kuwa katika kukabiliana na changamoto hizi Sekretarieti imeamua kuwekeza katika matumizi ya TEHAMA kwa kuanzisha Mfumo wa uzajaji matamko kwa njia ya Mtandao ili kurahisisha ujazaji wa matamko hayo.

Bw. Kipacha aliongeza kuwa mfumo wa ujazaji wa fomu za matamko kwa njia ya mtandao ni nyenzo ambayo itamuwezesha kiongozi wa umma kujaza tamko lake la rasilimali na madeni pamoja na tamko la mgongano wa maslahi nakuliwasilisha kwa Kamishna wa Maadili kwa njia ya mtandao na kwamba kupitia Mfumo huu kiongozi anaweza kujaza tamko lake akiwa mahali popote ambapo mtandao unapatikana.

Bw. Kipacha alifafanua kwamba, ujenzi wa mfumo huu waujazaji wa Matamko kwa njia ya Mtandao ulikamilika na kuanza kutumika kuanzia mweziAprili2020.Aidha, Mfumo huu unapatikana kupitia anuani ya https;//ods.ethicssecretaririat.go.tz aukupitiatovutiya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kubofya kitufe kinachosomeka “OnlinedeclarationSystem”.

Mafunzo hayo ya siku mbili yalitolewa na Wataalamu wa Mifumo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kitengo cha Kompyuta, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC) yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa Sekretarieti ya Maadili kuhusu matumizi ya Mfumo ili kuwawezesha kutatua shida mbalimbali zitakazojitokeza wakati viongozi wa umma watakapo wakijaza matamko yao ya mali na madeni kupitia njia ya Mfumo.