Wazazi na Walezi wametakiwa kuwalea watoto katka Misingi ya Maadili


Wazazi  na Walezi wametakiwa kuwalea watoto katka Misingi ya Maadili
05
Mar
2020

Wazazina Walezi wametakiwa kuwalea watoto katka Misingi ya Maadili

Wazazi na walezi wote nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanawalea watoto wao kwa kuzingatia misingi ya Maadili ili waweze kuwaViongozi na Watumishi bora wa hapo baadaye.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu Msaidizi Seketarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati Dodoma Bibi. Jasmin Bakari wakati wa Mafunzo ya Maadili kwa Watumishi wa Wakala wa Huduma za Manunuzi Serikalini (GPSA) mkoa wa Dodoma yaliyofanyika hivi karibuni.

“Katika kupanga mipango na mikakati kwaajili ya maendeleo ya kiuchumi ya haraka kwa nchi yetu, tunapaswa sasa kuweka mipango kwa ajili ya kuwajenga watoto wetu katika misingi ya Maadili Mpaka kwa vizazi vijavyo.

Aidha, Bibi Jasminalifafanua kuwa, malalamiko mengi yalipo katika jamiiyanatokana na Matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, wizi na utumiaji wa mihadarati mambo yote hayo yanasababishwa na mmomonyoko wa Maadili katika jamii zetu kuanzia ngazi ya familia.

“Awali wakati akiwasilisha mada ya Mgongano wa Maslahi kwa watumishi hao, Bibi. Jasmin alisema ni vyema watumishi wa umma wakajiepusha na vitendo vya mgongano wa maslahi kwakuwa madhara yake ni makubwa kwa taifa hali itakayopelekea rasilimali za nchi kunufaisha wachache na hivyo kupungua kwa uzalendo.

“Ndugu Watumishi wenzangu naomba tujiepushe na mgongano wa maslahi kama nilivyowaeleza njia za kuuepuka hapo awali kwakua jambo hili ni hatari kwa taifa letu. Baadhi ya madhara yake ni rasilimali za nchi kunufaisha wachache na hivyo kutokea kwa wimbikubwa la kundi la walio nacho na kundi la wasionacho. Hii inapunguza uzalendo na mwisho wake ni uvunjifu wa amani.”

Naye Meneja wa GPSA Mkoa wa Dodoma Bw. Presley Muro akitoa neno la kuhitimisha mafunzo hayo aliwataka Watumishi wenzake wa GPSA kuzingatia Maadili katika utendaji wao wa kazi kwani suala hilo ni la lazima na siyo la hiari katika Utumishi wa Umma.

“Akifafanua kuhusu uzito wa Maadili katika Taifa letu, Muro amesema kwakua suala la Maadili ni suala mtambuka ndio maana katika kila taasisi ya serikali katika Mpango Mkakakati wake ni lazima wahakikishe Watumishi wake wanapatiwa elimu ya Maadili ikiwemo rushwa.

“Naomba Watumishi wenzangu mtambue kuwa, mafunzo hayo ya Maadili hayajaletwa kwenu kwa ridhaa ya Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA au Meneja wa Mkoa, linatekelezwa kwa mujibu wa sheria na ndiyo maana wenzetu hawa waSekretarieti ya Maadili ni kazi yao kuhakikisha Watumishi wa Umma na Viongozi wanapata elimu ya Maadili na kuyatekeleza au kuyafuata Maadili husika.” Alisema Bw. Muro.

Hatahivyo Meneja huyo wa GPSA Mkoa wa Dodoma pia aliwaasa Watumishi wenzake kufanyakazi kwa misingi ya Maadili kwani bila kufanya hivyo mafunzo hayo hayatakuwa na maana kwao.

“Utekelezaji wa utoaji wa Mafunzo hayo ya Maadili kwa Viogozi na watumishi wa Umma ni moja ya jukumu la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kutimiza lengo lake la kusimamia na kukuza Maadili ya Viongozi nchini. Aidha, Katika Mafunzo hayo ya watumishi wa GPSA Mkoa wa Dodoma, mada ya Kanuni za Utendaji katika Utumishi wa Umma na Mada ya Mgongano wa Maslahi ziliweza kuwasilishwa.