Bw. Gerald Mwaitebele ,Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kaskazini Arusha (hayupo pichani) akiongoza kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 10/05/2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Mkoa wa Kilimanjaro.
Bi. Jasmin Awadh, Katibu Msaidizi Kanda ya Kati, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akitoa mada kuhusu mgongano wa masilahi na uwajibikaji wa pamoja kwa waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo. Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 8 Mei 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Chamwino.
Bi. Ester George, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, akitoa mafunzo ya mfumo ya ujazaji tamko kwa njia ya mtandao (ODS) kwa waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri hiyo. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino tarehe 8 Mei 2024.
Maafisa wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais,Sekretarieti ya Maadili Ya Viongozi wa Umma,Kanda ya Kaskazini-Arusha,Bw.Josephat Mkumbwa pamoja na Bi.Pendo Ulomi wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wapya wa Klabu ya Maadili iliyoko Arusha Girls Sec.School katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wakati wa ufunguzi wa Klabu hiyo Tarehe 25 April, 2024.
Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Onesmo Msalagi akitoa mafunzo kwa wanachama wa klabu ya maadili ambao ni wanafunzi wa shule ya sekondari Mwananchi iliyopo Halmashauri ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma. Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 24 Aprili 2024.
Bi. Rose Mugasha Afisa kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa uadilifu wanachama wa klabu za Maadili kutoka shule za msingi Nyasho A na Nyasho B wilayani Musoma Mkoa wa Mara. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika shule ya msingi Nyasho A tarehe 15 Aprili 2024.
Afisa Uchunguzi kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kaskazini Bi.Asia Erasto akitoa elimu kwa Wanachama wa Klabu ya Maadili ambao ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kaloleni iliyopo katika Kata ya Kaloleni Jijini Arusha .Mafunzo hayo yalifanyika shuleni hapo tarehe 16 Aprili,2024.
Wanachama wa klabu ya Maadili ambao ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nyanza wilaya ya Geita Mkoa wa Geita wakijengewa uwezo wa Maadili katika klabu yao na Bi. Abigail Majige kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa. Mafunzo haya yamefanyika tarehe 15 Aprili 2024 kwa klabu za Maadili zilizopo Shule za msingi na sekondari ndani ya Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga akishuhudia Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mhe. Fakii Lulandala, kilichoongozwa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini Bw. Gerald Mwaitebele. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara tarehe 05 Aprili 2024.
Baadhi ya maafisa uchunguzi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakifuatilia mada mbalimbali zinatolewa wakati wa kikao kazi cha uchunguzi kilichofanyika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha, tarehe 18 Machi 2024.