Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili. Hafla hiyo imefanyika Ikulu ya Chamwino Dodoma tarehe 24 Desemba, 2020.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Mhandisi John Kijazi (wa pili kushoto) akiongoza Kiapo cha Uadilifu kwa Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia. Hafla hiyo imefanyika Ikulu ya Chamwino Dodoma tarehe 24 Desemba, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi mara baada ya kumwapisha kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Dodoma tarehe 24 Desemba, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili (waliosimama nyuma) mara baada ya kumuapisha Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge, Kaimu Jaji Mfawidhi Dodoma Mhe. Latifa Mansuri, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Mhandisi John Kijazi, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deo Ndenjembi (Mb).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi mara baada ya kumwapisha kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Dodoma tarehe 24 Desemba, 2020.

Karibu


Sekretarieti ya Maadili ni Idara Huru ya Serikali chini ya Ofisi ya Rais iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Kazi yake kuu ni kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Na. 13 ya 1995 (Sura ya 398), hasa kufuatilia tabia na mienendo ya Viongozi wa Umma. Tovuti hii ni njia ya habari muhimu juu ya kukuza na kutekeleza kanuni na mambo ya kimaadili ambayo ni lazima yazingatiwe na Viongozi wote wa Umm... Soma zaidi

 • news title here
  24
  Dec
  2020

  Rais Magufuli amuapisha Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili, hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Dodoma... Soma zaidi

 • news title here
  15
  Dec
  2020

  Jaji Mkuu amlilia Kamishna wa Maadili

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma, hivi karibuni aliwaongoza waombolezaji kuuzika mwili wa Marehemu Mhe. Jaji (Mst.) Harold Reginald Nsekela jijini Mbeya... Soma zaidi

 • news title here
  11
  Dec
  2020

  Viongozi waaswa kusimamia Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu.

  Viongozi wote wanaosimamia utoaji wa huduma katika Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wanapaswa kuwajibika na kusimamia ipasavyo utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwenye maeneo yao... Soma zaidi

Habari Zaidi
  • 27
   Jul
   2017

   Sekretarieti ya Maadili yaadhimisha Siku ya Maadili.

   Mahali: At Mnazi Mmoja Stadium

   Soma zaidi
  • 29
   Jul
   2017

   maadili siku ya michezo

   Mahali: Gymkhana Ground

   Soma zaidi
  • 25
   Jul
   2017

   Warsha ya Wahariri wa Vyombo vya Habari

   Mahali: Serena Hotel

   Soma zaidi
  • 25
   Jul
   2017

   Baraza la Maadili

   Mahali: Karimjee Hall

   Soma zaidi
  Matukio Zaidi